× Home Ministries Choirs Pastors Bible Entertainment Development Health Love Fashion Music

Mwimbaji Sarah Adam Alianza kumtumikia Mungu kwa umri wa miaka chache

Category: International News  »  January 2024 »  Alice Uwiduhaye

Mwimbaji Sarah Adam Alianza kumtumikia Mungu kwa umri wa miaka chache

Mwimbaji Sarah Adam ni mwimbaji aliejulikana nchini Tanzania kwa nyimbo za kumsifu Mungu.

Sarah Adam ni mwabudu anayetoka nchini Tanzania, Dar es salama. Sarah ni mtumishi wa Mungu ni mwimbaji wa nyimbo za injili.

Yeye alizaliwa mkoa wa dodoma wilaya ya mpwapwa. Pia ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto saba. Amekuwa mtoto wa kwanza Kati ya hao saba (7). Kwa sasa ana Albam 3. Sarah alijulikana huko Nchini Tanzania kwa nyimbo yofauti za kumsifu Mungu.

Wakati alizungumza na paradise alisema haya " Wimbo wangu wa kwanza kuutoa ni mwaka 2012 ndio Mungu alitimiza kusudi lake ndani yangu la kuanza kumtumikia katika karama ya wimbaji.

Mimi nilikuwa napenda kuimba, jambo hakuwa sana na sikufahamu kama nitakuwa na huo wimbo binafsi wa kumwimbia Mungu maana niliimba katika kwaya ya kanisa ambalo nilikuwa Nasali, na kanisa lilikuwa chini ya mchungaji Adam ambaye ni babu yangu aliyemzaa baba yangu.

Nimeimba nikiwa na umri mdogo wangu kuanzia miaka 6 hadi 14, Ndio nilifunuliwa katika maono na Mungu kuwa nianze kumtumikia katika Wimbaji binafsi, ndipo nilianze kumtumikia Mungu nikiwa na miaka 16 ndio nilianza rasmi kutoa wimbo wangu wa kwanza ambao nilitoa mwaka 2012.

Namshkru Mungu akaniwezesha kuendelea zaidi na zaidi hadi sasa naendelea na kazi yake njema aliyoiweka ndani yangu nami najisikia furaha sana kumwimbia Yeye.

Aliendelea akisema "Lengo langu katika muziki na huduma ya wimbaji ninayoifanya ni kuimba nyimbo zenye ujumbe wa kuwatia moyo waliokata tamaa na waliopotea kuwarudisha kwa Yesu ndio Lengo langu hasa katika huduma ya wimbaji ninaoufanya ni watu waponywe na kubarikiwa kupitia huduma Mungu aliyonipa.

Jambo la kuwaambia Wapendwa wangu na wasomaji wa gazeti hili kwamba wamtafute Mungu kwa bidii na kuweka Tumaini lao kwa Mungu aliye juu maana yeye ndio chanzo cha baraka, uhai, mafanikio ndani ya maisha yetu na kama anachosema yeye kuwa yasiyowezekana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana;

Luka 1:37 Maisha ni fumbo, maisha ni kupanda na kusuka maisha ni Milima na mabonge, majaribu na raha changamoto na mengine mengi lakini utanindaje yote hayo ni kuweka Tumaini lako kwa Mungu naye atathibitika Kwaka.

Jambo la mwisho nawapenda wote na Mungu awabariki....Endelea kufatilia nyumbani zangu kupitia YouTube chanel...utakutana na nyimbo zangu pale nina Imani utabarikiwa Kuna mahali utaenda kupitia ujumbe wa nyimbo hizo, naomba msada pia kuweka like na subscribe pale ili uweze kupata nyimbo mpya zinazoendelea kuja ndani ya channel yangu ya YouTube na mitandao mengine yote ya kitambi.

Facebook napatikana kwa jina la Sarah Adam; YouTube..Sarah Adam; Instagram Offical Sarah Adam, na Napatikana kwa mawasiliano yangu ya simu kwa namba +255 683 954 520 Ahsante ..

Mwimbaji Sarah Adam Alianza kumtumikia Mungu kwa umri wa miaka chache

Tanga igitekerezo kuri iyi nkuru

pre-moderation

This forum is pre-moderated: your contribution will only appear after being validated by an admin.

Who are you?
Your post

To create paragraphs, just leave blank lines.