Mhubiri na mwimbaji maarufu wa muziki wa Injili kutoka Rwanda, Israel Mbonyi, ameachilia wimbo mpya uitwao “Unkebuke” tarehe 11 Novemba 2025.
Wimbo huu ni moja kati ya nyimbo 14 zinazounda Albamu yake ya tano “Hobe”, ambayo alizindua rasmi katika tamasha kubwa lililofanyika Intare Arena, Rusororo, mnamo tarehe 5 Oktoba 2025.
Wimbo huu mpya “Unkebuke” unaendeleza utambulisho wa Mbonyi kama mwimbaji wa nyimbo zenye ufunuo wa kiroho na sauti ya kipekee inayogusa roho za watu.
Maana ya Neno “Unkebuke”
Neno “Unkebuke” kwa Kinyarwanda linamaanisha “niinue, unifufue, unirejeshe tena.” Ni ombi la kiroho ambapo mwimbaji anamwomba Mungu amrudishe katika hali ya neema, ampe moyo mpya, na amjazilize kwa mafuta ya utumishi.
Wimbo huu ni sala ya toba, utakaso, na upyaisho wa moyo mbele za Mungu. Mbonyi anaimba kwa unyenyekevu mkubwa, akionyesha kiu ya roho ya kutaka kuishi karibu na Mungu pekee.
Maelezo ya Maneno ya Wimbo (Lyrics Translation na Ufafanuzi)
Verse 1
Uwiteka we, Urondore umutima w’umugaragu wawe mwami
Ee Bwana, chunguza moyo wa mtumishi wako mfalme wangu.
Umvugutire, Umpindure igikoresho gukwiye munzu yawe
Nisafishe, uniongoze niwe chombo kinachofaa katika nyumba yako.
Kuko aho uri, Ariho honyine nanjye nifuza kwibera
Kwa maana pale ulipo, ndipo nami natamani kukaa daima.
Ujumbe: Ni ombi la mtumishi wa Mungu anayetaka moyo wake uchunguzwe, utakaswe, na kuandaliwa kwa kazi ya Mungu.
Chorus
Unkebuke mwami, Mbone mumaso hawe,
Uniepushe Ee Bwana, niione uso wako.
Wuzuze amavuta mw’itabaza wampaye,
Nijaze mafuta katika taa uliyonipa.
Unsubizemo kunezezwa, Kunezezwa nagakiza.
Nirudishie furaha ya wokovu wangu.
Ujumbe: Kama ilivyoandikwa katika Zaburi 51:12, mwimbaji anaomba Mungu arejeshe furaha ya wokovu, na kumjaza tena Roho wake Mtakatifu.
Verse 2
Umpe kuzinukwa Ingeso zose za kamere ndusheho kukwegera,
Nipe kuchukia tabia zote za kimwili, nikukaribie zaidi.
Unkubitire Ibyaha Byose bimpeza kure Yu bwiza bwawe.
Niadhibu dhambi zote zinazoniweka mbali na utukufu wako.
Unkangurire Gusa na Kristo mw’ijambo no mubingerageza.
Nifanye nifanane na Kristo katika neno lako na majaribu.
Ujumbe: Hapa Mbonyi anatafuta utakaso wa ndani na nguvu za kushinda majaribu, akitamani kuwa mfano halisi wa Kristo.
Verse (Solo)
Naho ibyaha byanjye byatukura cyane, Ubasha rwose kubyeza byose.
Ingawa dhambi zangu ni nyekundu sana, Wewe waweza kuniosha zote.
Kandi nubwo njyewe ntagira shinge na rugero, Warandimiye Umpa andi mahirwe.
Hata kama sina msingi wala kipimo, umenichagua na kunipa nafasi nyingine.
Ujumbe: Ni tangazo la neema ya Mungu, kwamba hakuna dhambi kubwa sana isiyosameheka.
Bridge
Umpindure igikoresho, Gokoreshwa iby’umumaro,
Nibadilishe niwe chombo chenye faida kwa kazi yako.
Unyeze Kandi unyuzuze Kunezezwa nagakiza.
Nisafishe na kunijaza tena furaha ya wokovu.
Ujumbe: Ni hitimisho la toba na utii, ambapo mwimbaji anajiweka mikononi mwa Mungu ili atumiwe kwa utukufu wake.
Maoni ya Jumla
“Unkebuke” ni wimbo wa kiroho wenye maneno mazito yanayogusa moyo wa kila Mkristo anayetamani kubadilishwa na Mungu. Mbonyi anaendelea kuthibitisha kuwa muziki wake ni huduma ya Injili inayozidi kupenya mipaka ya Afrika Mashariki.
Kupitia albamu yake ya “Hobe”, ambayo ina nyimbo kama “Sindekura, Sijamalizana Nawewe, Hobe, Umurage, Kuna Uzima”, anathibitisha ubora wake katika kutengeneza muziki wa ibada wa kiwango cha kimataifa.
Miongoni mwa nyimbo zilizomfanya Israel Mbonyi kujulikana na kupendwa sana ni kama “Nina Siri,” “Baho,” “Nk’uduteze Imbere,” “Icyambu,” na “Mbwira.”
Nyimbo hizi zimegusa mioyo ya watu wengi kwa ujumbe wake wa imani, faraja na matumaini. Sasa, amekuja na wimbo mpya uitwao “Unkebuke,” unaoendelea kugusa watu wengi kwa maneno yake yenye nguvu za kiroho.
Kupitia “Unkebuke,” Israel Mbonyi anatukumbusha kwamba Mungu bado anaweza kutuinua hata baada ya kushindwa, anatupenda licha ya mapungufu yetu, na anatupa nafasi ya pili.
Ni wimbo wa kutafakari, wa maombi, na wa toba ya kweli — wimbo unaosisitiza ukuu wa rehema za Mungu.
Tazama wimbo “Unkebuke” wa Israel Mbonyi kwenye YouTube