× Home Ministries Choirs Pastors Bible Entertainment Development Health Love Fashion Music

Shukrani kwako Baba! Sikia Wimbo mzuri uitwayo "God of Miracles" na Aline Gahongayire

Category: International News  »  February 2024 »  Alice Uwiduhaye

Shukrani kwako Baba! Sikia Wimbo mzuri uitwayo "God of Miracles" na Aline Gahongayire

Gahongayire Aline ni mwimbaji ambaye ni maarufu sana katika nyimbo za kusifu na kumwabudu Mungu. Aline Gahongayire alianza kuimba na kucheza katika kutaniko ambako alifunzwa na nyanyake mama yake.Huko aliendelea kuimba katika kwaya ya Asafu ya kutaniko la Zion Temple.

Mwimbaji Aline Gahongayire alizaliwa Desemba 12, 1986 nchini Rwanda katika wilaya ya Kamonyi katika jimbo la kusini na ni mmoja wa ndugu wanne. Mwimbaji huyu ametoa Wimbo mpya katika kiengereza na kiswahili unaoitwa "God of miracles". Ni Wimbo mzuri sana unaoleta watu karibu na Mungu.

Kuna pale anapoimba:
Waweza yote
Waweza yote
Mwenyezi Mungu
Unaweza yote

Uzima Wangu
Ni ushuhuda
Kwa yote umetenda
Nashukuru Tena

Aline Gahongayire anajulikana kwa kusaidia wasanii na wasanii chipukizi. Miongoni mwa waliosaidia kuinuka na kuwa maarufu, tunaweza kumtaja msanii Niyo Bosco na pia walitengeneza wimbo uitwao "Izindi mbaraga".

Aline Gahongayire alianzisha shirika lisilo la faida "Ndineza Organization" kwa ajili ya kusaidia wasiojiweza. hasa watoto na wanawake.

Aline Gahongayire ni mwimbaji maarufu, mtunzi wa nyimbo, mzungumzaji, na mmoja wa viongozi wa ibada nchini Rwanda. Ana kipawa cha kusifu na kuabudu, na bado anatafuta kiwango kipya cha kuabudu maishani mwake.

Nyimbo zake Ndanyuzwe, Niyo yabikoze, Nzakomeza, Izindi mbaraga, Ntabanga, Hari impamvu Pe, Amen, Yarahabaye, Umwami Yesu, Iyabivuze, Warampishe, Umukiza wanjye ariho na kadharika

Tanga igitekerezo kuri iyi nkuru

pre-moderation

This forum is pre-moderated: your contribution will only appear after being validated by an admin.

Who are you?
Your post

To create paragraphs, just leave blank lines.