Injili Bora inafanyia kazi ya mwinjilisti katika kanisa la EPR-Gikondo/Karugira Sasa imetoa wimbo uitwao "Mwokozi".
Baada ya kurekodi nyimbo mbalimbali nchini Kenya sasa hivi lnjili Bora itoa nyombo wamepatia katika tamasha walikuwepo kwa Siku chache zilizopita ilikuwa tamasha ya kurekodi na video. Ni tamasha lililofanyika Juni 9, 2024, saa 9:00 alasiri katika Kanisa la Hope in Christ. Nyimbo mbili zimetolewa hadi sasa.
Kwenye tarehe ya 29 juni ndipo kwaya hii imetoa wimbo mzuri ambao umeitwa "Mwokozi". Wimbo huu umekuja baada ya ule unaoitwa "Hashimwe Yesu"
Katika Mwokozi wanasema: "Alipoteswa Yesu peke katika Gethsemane akakinywea kwa upendo kikombe cha uchungu. Mwokozi wangu alichukuwa yote, uzima wake alitoa kutuokoa alitufilia.
Akasimama peke yake kuchekwa na kupigwa uchwani akatiwa taji iliyo ya miba .
Akachukua msalaba njiani kwa Goligotha na akajeruhiwa sana kwa ajili yetu sisi.
Kwaya lnjili Bora ilianza historia yake mwaka 1997 ambapo ilianza na waimbaji 4 lakini sasa wamejitanua na kufikia waimbaji zaidi ya 100. Kwaya ya lnjili Bora wana lengo la uinjilisti, kila wanachofanya wanataka habari njema ya Yesu Kristo ifikie ulimwengu wote kwake, kwa wale wanaomjua ni kuwatia nguvu na kuwashirikisha habari za safari hii na wale wasiomjua Yesu na kuhubiri ujumbe.
Injili Bora wana albamu 6 ambazo ni "Amasezerano", "Heri", "Mana Ndaje", "Nzakambakamba", "Operation", "Kapernaumu". Albamu hii ya mwisho ni albamu iliyotengenezwa nchini Kenya katika uinjilisti wa injili ya Bora Nyimbo 4 zimetolewa kwenye albamu hii na zimesalia takriban 9 zaidi.