× Home Ministries Choirs Pastors Bible Entertainment Development Health Love Fashion Music

Fahamu kwa Kiswahili: Wimbo “Ibendera” wa Alicia na Germaine unaendelea kuteka mioyo katika East Africa

Category: International News  »  1 month ago »  Jean D’Amour Habiyakare (Amourkare)

Fahamu kwa Kiswahili: Wimbo “Ibendera” wa Alicia na Germaine unaendelea kuteka mioyo katika East Africa

Alicia na Germaine wametoa wimbo mpya “Ibendera” unaendelea kupendwa na wakaazi wa nchi za Afrika Mashariki (EA: East Africa).

Ingawa wengi hawasikii Kinyarwanda, mtindo wa Amapiano uliotengenezwa kwa ubunifu unafanya wimbo huu kupendwa hata na wale wasiopata Kinyarwanda.

Ndiyo sababu tulitengeneza maneno ya wimbo huu kwa Kiswahili, ili wale wengi wanaoupenda ambao wako katika eneo lote la Afrika Mashariki waweze kuusikiliza na kuufurahia. Ni wimbo mpya wametoa karibu, unaoitwa “Ibendera”, uliotoka rasmi tarehe 14 Januari 2026 ukiwa na video yake.

Hii ni makala ya kiroho inayoelezea na kuwasilisha lyrics za wimbo “Ibendera” za Alicia na Germaine kwa Kiswahili.

Sehemu ya 1 (Part 1)

Njye nabyirukanye iyo ntwaro
[Mimi nilikimbia na silaha ile]
Yanshishije ukubiri n’ikimwaro
[Ilinilinda aibu]

Ndetse n’imitwaro yandi ku mugongo
[Hata mizigo yangu hiyo ilikuwa mgongoni]
Iyo ntayigira ngo inkingire nari gupfa naburiwe nk’impongo
[Kama nisingekuwa nayo ilinilinda, ningekufa ingawa nilikuwa nimeonywa, kama swala.]
Mu miraba y’ibinduta
[Katika mikondo ya vurugu]

Urukuta rwakataraboneka
[Ukuta thabiti]
Rurabitangira ndarokoka
[Unaonikinga hunifanya niokoke]
Ari rwo ntwaro
[Ndiyo hiyo silaha]
Y’ikitabashwa yampaye amahoro
[Silaha isiyoshindwa ilinipa amani]

Inkomoko yayoo
[Asili yake]
Ni kuri Kristo
[Ni kwa Kristo]
Niwe gitambo
[Yeye ndiye sadaka]
Yanguze amaraso
[Alinunua kwa damu]

Iyo ankuraho amaso
[Anaponiondolea macho]
Ndetse nibitekerezo
[Hata mawazo]
Ubu nanjye mba nitwa ikirumbo
[Kwa sasa, ningeliitwa mtu asiye na faida, lakini haikuwa hivyo.]

Pre-Chorus

Sinkibarizwa mu banyabwoba
[Sihesabiwi miongoni mwa waoga]
Kuko nahawe impano
[Kwa sababu nilipewa zawadi]
Y’umwuka wera
[Ya Roho Mtakatifu]

Chorus

Mbumbatiwe nibiganza
[Nimekumbatiwa kwa mikono]
Bya rurikanwa
[Ya umaarufu]
Umwami uhora aganza
[Mfalme anayekaa akitawala]
Eee ntazemera
[Ee hatakubali]

Ko izina ry’iwe ritukwa
[Jina lake litukanwe]
Ibendera rye ntirizigera rimanurwa
[Bendera yake haitashushwa kamwe]

Sehemu ya 2 (Part 2)

Uwo mvuga ni we rukundo nyarwo
[Yule ninayemzungumzia ndiye upendo wa kweli]
Uko byagenda kose ntazambabaza
[Bila kujali jinsi itakavyokwenda, hataniumiza]

Satani akeka ko amfite wese
[Shetani anafikiri amenishika kabisa]
Akirengagiza ko nta bubasha afite ku bugingo bwanjye
[Anasahau kuwa hana mamlaka juu ya maisha yangu]

Ndi nde wo gutoneshwa bigeze aha
[Nani wa kupendelewa kufikia hapa]
Umuhemu nkanjye simbikwiye
[Msaliti kama mimi sitastahili]

Bridge

Ibikomere ntibyambuza kumugwa inyuma
[Majeraha hayatanizuia kumfuata nyuma]
Njye ndabizi aranzirikana
[Mimi najua ananikumbuka]

Yansubije agaciro namburiwe mu maganya
[Alinirudishia thamani niliyopoteza katika mateso]
Mu maganya ankunda ntaburiganya
[Katikati ya mateso, ananipenda bila udanganyifu]

Wimbo huu una ujumbe mfupi lakini mzito wa ushindi wa kiroho, ukisisitiza kuwa bendera ya Mungu haiwezi kushushwa, hata katikati ya majaribu na vita vya maisha. “Ibendera” ni wimbo wa kutia moyo, kuimarisha imani na kukumbusha waumini kuwa ushindi wao uko ndani ya Kristo.

Mbali na “Ibendera”, Alicia na Germaine wanajulikana pia kupitia nyimbo nyingine zilizopendwa sana kama “Ndahiriwe”, “Uriyo”, “Ihumure”, “Wa Mugabo”, “Rugaba” na “Urufatiro”, ambazo zimegusa mioyo ya watu wengi ndani na nje ya Rwanda.

Kwa ujumla, Alicia na Germaine wanaendelea kuwa sauti muhimu katika muziki wa Injili, wakibeba ujumbe wa tumaini, imani na sifa. Kupitia nyimbo zao, wanaendelea kuinua bendera ya Mungu na kuhamasisha wengi kuendelea kumwabudu kwa moyo wote.

Tazama wimbo ‘Ibendera’ wa Alicia na Germaine kwenye YouTube

Tanga igitekerezo kuri iyi nkuru

pre-moderation

This forum is pre-moderated: your contribution will only appear after being validated by an admin.

Who are you?
Your post

To create paragraphs, just leave blank lines.